×

Hukumu Kesi Ya Evans Aveva na wenzake Kutolewa Saa Nane

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu ya kesi inayomkabili Rais wa zamani wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na wenzake baada ya kutajwa mida ya saa tano na kuahirishwa hadi saa nane kwa ajili ya kutolewa hukumu hiyo.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simb. Mbali na Aveva washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Godfrey Nyange (Kaburu) ambaye alikuwa Makamu.

 

Katika kesi hiyo, upande wa mashitaka ulikuwa na jumla ya mashahidi 10 na vielelezo mbalimbali huku washitakiwa wakijitetea wenyewe.

 

Mashtaka hayo ni pamoja na yakula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kutoa maelezo ya uongo.

 

Katika shitaka la kughushi linawakabili  washitakiwa wote, wanadaiwa walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola 40,577 sawa na zaidi ya Sh milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli.

 

Pia katika mashitaka mengine inadaiwa Aveva na Nyange  kati ya Machi 10 na Septemba 30 mwaka 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.

Leave a Comment