

MENEJA Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc Alex Bitekeye (kushoto) akionyesha tuzo ambayo kampuni ya Vodacom Tanzania Plc ilikabidhiwa baada ya kuibuka kinara katika sekta binafsi kwa mchango wake katika maendeleo ya jamii kwenye wiki ya Azaki ambao ulifanyika jijini Dodoma hivi karibuni. Kulia ni Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima.