×

Mondi Ampongeza Alicia Keys Kumshirikisha Albamu Yake

 

 

MWANAMUZIKI staa wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz, amemtumia ujumbe wa kumpongeza mwanamuziki  wa Marekani, Alicia Keys, kutokana na kumpa fursa ya kushiriki katika albam yake inayotarajiwa kutoka karibuni.

Amempongeza mwanamuziki huyo wa muziki wa R&B  na mwanamuziki Swizz Beatz kupitia akaunti yake ya Instagram, akiwashukuru kwa kumpa nafasi hiyo adimu.

Hata hivyo, mashabiki wa Diamond, kupitia mitandao mbalimbali,  wanahisi nyota huyo aliyeipa nchi yake na Afrika Mashariki umaarufu katika muziki, alistahili kupeta nafasi hiyo.

Wakati huohuo, habari hiyo imetokea kipindi kifupi baada ya mzazi  mwenzake na staa huyo, Tanasha Donna, mrembo, raia wa Kenya, kumvaa mwanamziki wa kike Mtanzania, Zuchu, na Diamond, akidai “waliiba” maneno ya wimbo wake wa Radio.

 

Leave a Comment