×

Sakata la Maji! Aweso Apita Mtaa kwa Mtaa

BAADA ya kazi kubwa usiku na mchana kuhakikisha maji ya mto Ruvu yanafika mitamboni na kuepusha Shughuli za binadamu tenki letu la chuo kikuu ambalo mara ya mwisho kuwa na maji baada ya changamoto ya ukame kuanza ni tarehe 11 mwenzi wa 10.

Mapema leo Waziri wa Maji Jumaa Aweso amefungua mtambo wa tenki la chuo kikuu kuruhusu Maji kwenda Maeneo ya Survey, Masaki, Mikocheni, Kawe, Tageta, Mbweni, Makumbusho, Kijitonyama, Mwananyamala, Mjini Kati.

Jana usiku kulifanyika zoezi la ufunguaji wa maji katika Bomba kuu la usambazaji linaloelekea ukanda wa Magomeni baada ya kufungulia maji toka kwenye tenki.

Huduma ya Maji ilifika katika maeneo tajwa kwa muda wa masaa 8 kuanzia saa 3 Usiku ambayo ni;Shekilango, Urafiki, Mabibo, Manzese, Sinza, Magomeni.

“Niwaombe sana kipindi hiki tuhifadhi Maji kwa wingi na zaidi niwasihi sana tuwe wamoja kuliko kipindi chochote kile, watumishi wa DAWASA na Wizara ya Maji tuwe imara tupambane kwa uwezo wetu wote, viongozi wa dini kesho siku ya ibada tuiombee nchi yetu kupata baraka ya mvua na naamini tutavuka salama kipindi hiki kigumu.”
Amesisitiza Waziri Aweso.

 

Baada ya zoezi hili Aweso ameingia mtaani kuhakikisha iwapo maeneo haya yamefikiwa na MajI na kukutana na Wananchi waliothibitisha kuwa Maji yapo tayari kwenye maeneo yao baada ya kukosekana muda mrefu kutokana na kina cha maji kupungua kiasi cha kushindwa kusukuma maji kufika maeneo hayo.

Leave a Comment