MWANAMUZIKI mahiri wa Rhumba, Le General Defao Matumona (62) amefariki Desemba 27, 2021 akiwa Douala, nchini Cameroon.
Defao ni mwanamuziki mwenye kipaji cha kutunga na kuimba kwa sauti nyembamba na nyororo, alizaliwa Disemba 03, 1958, Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Defao amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi akiwa Nchini Cameroon.
