
HUYU anaitwa Aslay Isihaka Nassor kijana aliyezaliwa Mei 6, mwaka 1995 wilayani Temeke mkoa wa Dar es Salaam na baadae kuibukia kwenye muziki akiwa na umri mdogo kabisa. Wakati wa harakati zake, Aslay alitoa kibao alichokipa jina la ‘Naenda Kumwambia Mama’ na kufanikiwa kupata mapokezi mazuri kwa washabiki wa muziki wa Bongo Fleva.
Baadae akatoa wimbo mwingine aliyomshirikikisha Mhe. Temba alioupa jina la ‘Na Wewe’. Aslay akaendelea kutingisha vichwa vya muziki we Bongofleva nchini kipindi hiko kama Diamond, Ney wa mitego na Alikiba. Aslay alifanya mambo makubwa katika umri mdogo. Alifanya muziki huku akiwa shule ya sekondari.
Matokeo ya mwisho ya mitihani wa kidato cha nne yakatoka na bahati mbaya Aslay alifeli na hapo akaamua kukazana kwenye muziki ili aweze kutumiza ndiyo zake. Muziki ukamkubali akafanya vyema na hata kumshawishi Mkubwa Fella kumchukua na kumuunganisha na vijana wenzake watatu kuunda Kundi la Yamoto Band.
Akiwa Yamoto Band, Aslay alifanikiwa kushirikiana na wenzake kutengeneza vibao vya Moto ambavyo vilitokea kuwa vibao pendwa. Vibao kama Ntajuta, vilitikisa kwenye kiwanda cha muziki nchini Tanzania. Wakapata shoo za maana ndani na nje ya nchi na kujiingizia kipato cha kutosha.
Kipindi ambacho Aslay alipokuwa kwenye kilele cha mafanikio alifanikiwa kumsaidia mama yake pesa za matumizi na hata kumpa mtaji wa biashara. Aslay alikuwa anampenda mama yake mno kiasi kwamba kila Jambo alokuwa anataka kulifanya ilikuwa lazima amshirikishe mama yake aliyekuwa anaitwa Moza.
Mwaka 2015 Aslay alipata pigo la kuondokewa na mama yake mzazi. Bi Moza aliyefariki dunia Septemba 2015 na kumuachia simanzi kubwa kwenye maisha yake. Kuonyesha mapenzi makubwa kwa mama yake aliamua kumpa jina la mama yake mtoto wake aliyebahatika kumpata na mwanamke mmoja aliyekuwa anajulikana kama Tessy.
Mwaka 2018 Aslay aliamua kuandika barua ndefu kwenda kwa mama yake. Barua hiyo ilikuwa na maneno ya kuhuzunisha na kuonekana kumkumbuka vilivyo mama yake. Aslay aliandika barua hiyo kwenda kwa mama yake ikiwa imepita miaka miwili tangu mama yake aiage dunia.
Hellow Mama najua unanisikia mwanao tangu uondoke life its so complicated kuliko nilivyodhania, kila kitu kwangu tabu nakosa sana ushauri wako natamani kuongea nawe japo hata siku moja lakini nafahamu kwa mapenzi ya Mola haiwezekani nakuombea kila la heri huko ulipo.
Japo kwasasa nimepata kibinti pacha wako, jina lake nimemuita Mozza I wish ungemuona mmefanana sana. Kuna kitu Mama nataka kukugusia juu ya ndoto yangu bado sana natamani kuwa msanii mkubwa kama Kaka zangu na Dada zangu walionitangulia kwenye Muziki. Ndoto niliyokuwa nakusimulia kila wakati tukila Chakula cha jioni.
Mama Kila kukicha Wananirushia mawe nisifike niendapo. Mawe yote Mama nimeyaokota najengea barabara nifike niendapo, hakuna wakunifuta mimi machozi yangu nalia kilio cha mtu mzima maumivu ndani kwa ndani.
Juzi nilitamani nikupigie simu nikuambie yanayonisibu mwanao, Namba yako haipatikani labda umeweka call busy unaniombea dua njema. Nimuambie nani yanayonisibu ndani ya Moyo wangu juu ya Mziki wangu na maisha yangu?
Mashabiki wangu ndiyo wananipa Ujasiri wa kupambana na kukomaa hivo hivo. Sikufaidika na kile nilichokifanya kwa zaidi ya miaka 15. Hata mimi ukiniuliza ilikuwaje nakosa cha kukujibu Mama nataka tukae kikao cha dharura, tuone ilikuwaje.
I feel inferior, najihisi mnyonge, Nawaza nitaanzia wapi?. I just feel hopless and more hopeless day by day. I dont know. Kila ninaposhika panageuka mwiba mchungu kwangu. Natamani kujua kama unafahamu nanyanyaswa kisa Muziki wangu.
Kiukweli Mama siwezi kulalamika sanaa maana hata wakati napokuwa mpweke mashabiki zangu huniliwaza kwa kusapoti kazi zangu wamekuwa ndiyo faraja kwangu. Ndiyo wananifanya niwe jasiri wa kuwatengenezea Muziki mzuri kila kukicha. Sometimes nikiwaza mwanangu ataishije, na familia nitaitunza vipi, bila Muziki?
Natumaini utanijibu basi hata ndotoni Mama kama barua yangu utaipokea.
Nimekukumbuka sana mwanao
Aslay.
Nakupenda Mama.”
Mwaka 2019 Aslay alionekana kumkumbuka tena mama yake kwa kutumbuiza kibao cha Angekuwepo mama na kwenda kumuomba mama yake Nandy awe mama yake wa hiari. Aliimba kwa hisia nyimbo hiyo na kuuliza ukumbi wote. Mapenzi kwa mama yake yamekuwa makubwa tofauti na baba yake kwani mara kidogo ameonekana kumtaja baba yake.
Aslay anaendelea kufanya shughuli zake za muziki huku akiwa amefanikiwa kupata watoto wawili wa kike mmoja akiitwa Moza Aslay na mwingine ambaye kumpata jina imekuwa ngumu. Aslay ambaye hivi sasa anatamba na wimbo alioshirikishwa na Mr Blue maarufu kama Kabyser.