×

Wachapana makonde kisa Gazeti la Championi

Shinda Nyumba na Global (14)Wafanyakazi wa Global Publishers wakati wa uzinduzi wa Shinda Nyumba katika ofisi za Global Bamaga , Mwenge.

Aplina Philipo, Mbeya
SHINDANO la bahati nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers, juzi lilisababisha ‘majibaba’ wawili kurushiana makonde kisa kikiwa ni kugombea Gazeti la Championi ambalo lina kuponi maalum ya bahati nasibu hiyo.
Tukio hilo la aina yake lilitokea maeneo ya Kituo cha Daladala cha Kabwe jijini hapa, ambapo wanaume hao ambao majina yao hayakupatikana, walifanya umati uache shughuli zao na kushuhudia pambano hilo kwa muda.
Ilikuwa hivi, mmoja wa wahusika hao ambaye ni mpigadebe wa daladala kituoni hapo, alikuwa ameshika gazeti hilo, akatokea mtu mwingine akalichukua, wakati huo yule mpigadebe alikuwa bize akitafuta kalamu ili ajaze kuponi inayopatikana ndani ya gazeti hilo kwa ajili ya kujishindia nyumba.
Sekunde kadhaa baadaye ukaibuka mzozo kutokana na wahusika hao kuanza kuligombania gazeti hilo, hali hiyo ikasababisha mzozo zaidi kiasi cha kufikia hatua ya kurushiana makonde, lakini waliwahiwa na raia wema waliowaamua.
Kilichobaki ni wawili hao kurushiana maneno huku kila mmoja akimshutumu mwenzake kuwa anashindwa kununua gazeti la shilingi mia tano tu. Lakini mwisho wa mvutano huo ni kuwa mpigadebe aliondoka na gazeti.

Leave a Comment