
DIAMOND Platnumz; ni nembo ya muziki wa Tanzania ambaye kupitia EP yake mpya ya First Of All (FOA) ameibua mambo mengi ambayo bado mashabiki wanayajadili.
Miongoni mwa mambo hayo ni mashairi ya Wimbo wa Nawaza ambapo amezungumza kuhusu msongamano wa mawazo kichwani mwake.
Diamond au Mondi anazungumzia jinsi ambavyo amekuwa akisumbuka kuhusu sababu ya ugomvi wake na King Kiba.Kisha akagundua kuwa yote ni ushamba na kutokomaa.
“Nilowaza leo nishawaza sana mi na Kiba ugomvi kipi, nikagundua ni ushamba na ujana wa kugombania mashabiki,” anasema Diamond na kuibua hisia kwamba huwenda hataki tena ugomvi na Kiba.
Ugomvi wa Diamond na Kiba umedumu kwa miaka mingi ambapo mara zote umekuwa ukichochewa na mashabiki wao; kila upande ukijiona ni bora zaidi ya mwingine.
sifael paul