×

Ajali ya Gari Yaua Watu 6 na Kujeruhi Wengine Wanne Wilayani Monduli.

Noah baada ya kupata ajali

WATU sita wamefariki na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Alkatani, Monduli mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo ikihusisha Noah namba T 189 DFY na lori (Scania).

Lori aina ya Scania lililopata ajali

Jeshi la Polisi linamshikilia dereva wa lori hilo baada ya uchunguzi wa awali kuonesha uzembe wa kushindwa kufuata alama za usalama barabarani pamoja na mwendokasi ndiyo chanzo cha ajali hiyo.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori ambaye alishindwa kulimudu gari

Leave a Comment