×

Zaidi ya Wanajeshi 1000 wa Ukraine Wamesafirishwa Kwenda Urusi

Eneo la Viwanda la Azovstal Steel Plant ambalo walilokuwa wamejificha wanajeshi wa Ukraine

WANAJESHI zaidi ya 1000 kutoka katika Jimbo la Mariupol waliojisalimisha kwa majeshi ya Urusi watasafirishwa kwenda Urusi kwa ajli ya Uchunguzi.

 

Hayo yamethibitishwa na Shirika la Utangazaji la Taifa TASS siku ya Jumatano.

Jimbo la Mariupol limeshambuliwa vikali na majeshi ya Urusi

Chanzo hicho kimethibitisha kuwa Urusi inajiandaa pia kusafirisha idadi nyingine ya wafungwa wa kivita katika mipaka ya nchi yake.

 

Mwishoni mwa mwezi Mei Waziri wa Ulinzi wa Urusi alithibitisha kuwa Zaidi ya wanajeshi 1000 wa Ukraine walijisalimisha baada ya mapigano makali katika jimbo la Mariupol kwenye eneo la Viwanda la Azovstal Steel Plant.

 

Hadi sasa Mamlaka za Ukraine hazijatoa tamko lolote kuhusu taarifa iliyotolewa na Shirika la Utangazaji la TASS.

Leave a Comment