×

Raia wa Uingereza Wafariki Dunia Nchini Bangladesh kwa Kupewa Sumu

Rafiqul Islam 51 pamoja na mwanaye Mahiqul 16 raia wa Uingereza wameripotiwa kufariki nchini Bangladesh

BABA Pamoja na Mtoto wake raia wa Uingereza wamefariki dunia nchini Bangladesh kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni sumu kama alivyoripoti msimamizi wa Polisi nchini humo Farid Uddin.

 

Rafiqul Islam mwenye umri wa miaka 51, na mwanaye Mahiqul mwenye umri wa miaka 16, walipatikana wakiwa wamepoteza fahamu pamoja na watu wengine kwenye familia yao siku ya Jumanne Alasiri.

 

Baadaye wote wawili walifariki wakiwa njiani kupelekwa hospitali, huku mke wa Islam aliyejulikana kwa jina Husnara 45 na Watoto wao wengine wawili wakipelekwa Hospitali.

Ibada Maalum ya kuwaombea watu hao waliofariki imefanyika nchini humo

Watoto hao wengine wawili walijulikana kwa majina Samira 20 pamoja na Sadiqul 24 wakitibiwa, Husnara na Samira bado wapo katika hali mbaya huku Sadiqul akitajwa kuwa anaendelea vizuri na bado anapatiwa matibabu zaidi.

 

Msimamizi wa Polisi wa Bangladesh alinukuliwa akisema

 

“Baada ya kujadili hali ya jumla Pamoja na Madaktari na kukagua eneo la tukio, tunaamini kuwa hii inaweza kuwa ni kesi ya Sumu. “

Watu hao wamefariki kabla hata ya kufikishwa Hospitalini

Familia hiyo kutoka Cardiff huko Uingereza, walikuwa wamekuja katika likizo ya miezi miwili ambapo walikuja nchini Bangladesh kuwatembelea Jamaa zao wa nchini humo ambapo walikuwa wamekodisha nyumba katika Jiji la Sylhet lililopo Nchini Bangladesh.

 

 

 

 

 

Leave a Comment