×

Man United Yatoa Tamko Juu ya Hatma ya Ronaldo, Ni Baada ya Kichapo Dhidi ya Brentford

Mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo

BAADA ya kupoteza mechi dhidi ya Brentford kwa mabao manne kwa sifuri watu wengi walitaka kusikia nini kitatokea juu ya mshambuliaji wa timu hiyo Cristiano Ronaldo.

 

Mfululizo wa matokeo mabaya umezidi kumuweka Ronaldo katika hali ngumu ikizingatiwa kuwa alihusishwa na kuomba kuachana na klabu hiyo

 

Mshambuliaji huyo wa Kireno ambaye amepata mafanikio mengi katika mpira wa miguu anataka kushiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya.

Ronaldo anatarajiwa kubaki katika viunga vya Manchester United licha ya kuomba kuondoka

Mchezaji huyo namba mbili kwa tuzo za mchezaji bora duniani ameshinda Ballon D’or mara tano nyuma ya Lionel Messi mwenye tuzo hizo saba.

 

Msemaji wa klabu ya Manchester united ya Uingereza ameendelea kusisitiza kwamba mchezaji huyo hauzwi na hakuna mabadiliko ya nafasi kwa mshambuliaji huyo ataendelea kuwa chaguo katika nafasi ya ushambuliaji.

 

Klabu ya Manchester United imeshika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi baada ya mechi mbili za kwanza kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1992.

Leave a Comment