
SAMAKI anayejulikana kwa jina la kingereza Electric Eel anayepatikana katika mto wa Amazon barani Amerika kusini ni moja ya Samaki wenye uwezo wa kuzalisha nguvu ya umeme mwilini mwake kwa kutumia organ maalum.
Samaki huyo anakadiliwa kuwa na uwezo wa kuzalisha nguvu ya umeme inayofikia volt 500 ni mara mbili ya umeme wa majumbani ambao ni volt 240, umeme unaozalishwa na Samaki huyo unaweza kuua viumbe mbalimbali kama binadamu hata mamba.

Samaki huyo hutumia nguvu hiyo kama silaha yake ya kujilinda dhidi ya maadui vilevile kupata vitoweo kama Samaki na wadudu wengine majini.