Mwanamama Sophia Wilson mkazi wa Paje visiwani Zanzibar, ameweka wazi kwa wanawake wote wanaodhani kuwa unapoolewa na Mzungu au kuwa naye kwenye mahusiano basi umemaliza kila kitu na shida zako zimeisha.
Amesema imani hiyo siyo kitu cha kweli ambapo siyo kweli kwa sababu kuna Wazungu wengine hawana fedha kabisa na wanahitaji mwanamke anayejishughulisha ili kusaidiana katika maisha.
Sophia ambaye anamiliki mgawaha unaojulikana kama Smoothie, unaouza ice cream waliozipa jina kuwa ‘ice cream za ajabu’ eneo la Paje visiwani humo amesema yeye ni mke wa Mzungu lakini anahangaika na biashara zake ili aweze kutoboa zaidi kimaisha.