
Dar es Salaam, 22 Julai 2023: Chuo kikuu Mzumbe kimehitimisha maonyesho na kujivunia kutoa wahitimu wengi ambao kwasasa ni viongozi wakubwa serikalini.
Akizungumza kwenye maonyesho ya 18 ya vyuo vikuu, Kaimu Makamu wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Profesa, William Mwegoha amesema udahili umekuwa ukiongezeka kila mwaka ni kutokana na matokeo ya juhudi ambazo wanazifanya timu nzima ya chuo hicho katika kuushawishi Umma kuwa wanatoa program nzuri zinazotoa matokeo mazuri ikiwemo upande wa sheria.

“Kwa upande wa sheria tunafundisha kwa vitendo kwa vitendo na hata vijana wanapokwenda kwenye shule ya sheria ya Law School huwa ni kati ya vijana ambao wanafanya vizuri sana.
Program yetu ni miaka mitatu ikilinganishwa miaka minne ambayo vyuo vingine vyote vinatoa lakini wanafunzi wanaotoka Mzumbe ni wazuri zaidi kwa vitendo na uwezo wa kufanya kazi.

Lakini maeneo mengine ambayo tupo vizuri ni upande wa utawala ambapo ni kati ya nguzo muhimu sana ni kufundisha viongozi upande wa rasilimali watu, upande wa usimamizi na utawala ambao kutokana na aina yetu ya ufundishaji ambapo wanafunzi wanakwenda kwenye mafunzo ya vitendo wanakwenda kwa muda mrefu, hivyo basi wanajenga uwezo wa ufanyaji wa kazi hata kabla ya kumaliza chuo hivyo wakitoka hapo inakuwa ni rahisi sana kupata ajira kwa sababu wanachukuliwa sana kwa ajili ya kujitolea na kupitia huko wanapata ajira amesema, Profesa Mwegoha.
Amesema kwa upande wa mahusiano mazuri waliyoyajenga kwenye makampuni, Viwanda na Taasisi mbalimbali ambazo zinachukua wanafunzi wao kwaajili ya kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo baada ya kutoka wanakuwa tayari kuingia kwenye soko la ajira au kujiajiri.
Maonyesho hayo ya 18 ambayo yameandaliwa na Tume Ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yalifunguliwa Julai 17, 2023, na yamehitimishwa leo, Julai 22, 2023 na Naibu Waziri Omary Juma Kipanga.