×

Hotuba Ya Mkuu Wa Kitengo Cha Huduma Kwa Wateja Wa Tigo, Mwangaza Matotola Wakati Wa Uzinduzi Wa Maadhimisho Ya Wiki Ya Huduma Kwa Wateja

Oktoba 2 2023 Iringa

Wageni waalikwa,

Waandishi wa Habari,

Mabibi na Mabwana,

Habari za Asubuhi!

  • Napenda kuwashukuruni nyote kwa kuungana nasi katika siku hii adhimu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja na leo ikiwa ni ufunguzi rasmi wa maadhimisho haya
  • Tigo inafuraha kuungana na watoa huduma ulimwenguni kote kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa wiki ya kwanza ya mwezi Octoba kila mwaka na kwa mwaka huu itaadhimishwa kuanzia tar 2– 9 Octoba.
  • Tigo inatambua kazi kubwa inayofanywa na team ya wataalam wetu wa huduma kwa wateja zaidi ya 1000, wanaohudumia wateja zaidi ya milioni 13 nchi nzima. Kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu “Team Service ”, inaonesha umuhimu wa watoa huduma wetu kufanya kazi kwa pamoja ili kutoa huduma bora kwa ufanisi kwa wateja wetu wote.
  • Kupitia wiki hii ya huduma kwa wateja, Tigo inadhamiria kukuza uelewa wa wateja wetu juu ya taaluma ya huduma kwa wateja na wakati huo huo ikitambua na kuwashukuru wataalamu wetu wote waliopo mstari wa mbele kutoa huduma zenye ubora kwa wateja wakati wote.
  • Tigo ni mtandao wa watu unaoongoza kwa ubunifu unaozingatia mahitaji ya wateja. Ubunifu huu unadhihirika katika namna tunavyohudumia wateja wetu kupitia njia mbalimbali kama; namba 100 – kuongea na muhudumu kwa wateja, namba 100 kujihudumia kwa njia ya sauti, mitandao ya kijamii na katika maduka yetu zaidi ya 52 nchi nzima.
  • Umahiri wa watoa huduma wetu pamoja na ubora wa huduma za Tigo umepelekea wateja wetu kuendelea kupendekeza huduma zetu kwa ndugu,jamaa na marafiki kwa kiwango cha juu cha asilimia 80. Tunawashukuru sana wateja wetu kwa kuendelea kutuamini.

Ndugu wageni waalikwa;

  • Kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu, hapa Tigo tunathamini sana mchango wa watoa huduma wetu na jinsi ambavyo wameweza kuendana na kasi ya mabadiliko, na kutokana na juhudi hizo tunaendelea kusisitiza kuwa kampuni itandelea kutoa huduma bora kwa wateja wetu kila siku kama ambavyo wafanyakazi wetu wa kitengo cha huduma kwa wateja walivyoweza kuonyesha umahiri wao katika mikoa yote nchini.
  • Wiki ya huduma kwa wateja itahitimishwa kwa kufanyika hafla ya utolewaji wa tuzo maalum kwa wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja. Tuzo hizo zitatolewa ili  kuwapongeza na kuwapa moyo wafanyakazi hao kwa kuendelea kutoa huduma bila kuchoka huku wakizingatia maadili ya kazi pamoja na ubora.

  • Napenda kuhitimisha kwa kuwapongeza wafanyakazi wetu kutoka idara mbalimbali, na wadau wetu kwa kuendelea kuwa sehemu ya mafanikio ya kampuni hii kwa kujitoa kwao na kuhakikisha tunafikia malengo yetu.
  • Tunawahakikishia wateja wetu kuwa tumejizatiti kuhakikisha tunatoa huduma zenye viwango vya Kimataifa na zenye kukidhi mahitaji yao.

Asanteni Sana!

Leave a Comment