×

Waziri Mkuu Aongoza Matembezi Kuhamasisha Ufanyaji wa Mazoezi Kuzuia Magonjwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 4, 2024 ameongoza matembezi ya kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi ill kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

Matembezi hayo ya kilomita 10 yalianzia Coco Beach jijini Dar es Salaam hadi mzunguko wa Hospitali ya Aga Khan kisha kurudi Coco Beach.

Akizindua mazoezi hayo, Waziri Mkuu Majaliwa amewapongeza wananchi kwa kujitokeza kushiriki mazoezi hayo kwakuwa yanajenga afya na yanasaidia kuepusha magonjwa yasiyoambukiza.

“Kipindi cha nyuma magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari na shinikizo la damu tulikuwa tunadhani ni magonjwa ya matajiri lakini siku hizi yanawaathiri watu wote, ikiwemo vijana na wazee hivyo inatupasa watu wote kuchukua hatua kukabiliana na magonjwa haya,” alisema.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kwa siku za hivi karibuni magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari na shinikizo la damu yamekuwa miongoni mwa magonjwa kumi yanayoongoza kuathiri Watanzania.
Mazoezi ya kila Jumamosi yaliyozinduliwa leo yatafanyika kupitia Barabara iliyopo pembezoni mwa fukwe, kuanzia eneo la Coco beach kupitia Daraja la Tanzanite hadi makutano ya Barabara ya Aghakan na kuelekea Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

Leave a Comment