
Washindi 10 wa droo ya kwanza ya Kampeni ya Tap Tap Utoboe inayoendeshwa na Benki ya Exim, wametangazwa leo na kukabidhiwa zawadi zao.
Washindi hao wametangazwa na Silas Matoi , Mkuu wa Idara ya Njia Mbadala za Kidijitali wa Exim Bank, na kueleza kuwa lengo ni kuwahamasisha wateja wa benki hiyo kufanya miamala yao kwa kutumia simu za mkononi na mtandao kufanya miamala ya malipo. 
Kampeni hiyo ya miezi mitatu inatoa washindi wa kila wiki na mwezi ambao wanajishindia fedha taslimu na mwishoni kutakuwa na washindi wa pikipiki, Bajaj na mshindi wa kwanza atajinyakulia gari mpya.
Droo hiyo ilifanyika Juni 19, 2024 katika Makao Makuu ya Exim Bank jijini Dar es Salaam.