
Jeshi la Polisi limewakamata na kuondoka na viongozi wa kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya viongozi hao kudaiwa kukaidi agizo la polisi la kutaka kutoandamana leo Septemba 23.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na mtoto wake Nicole wamekamatwa muda mchache kabla ya kuanza Maandamano eneo la Magomeni, Dar.
Vilevile Chadema imedai, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu alichukuliwa asubuhi ya leo Nyumbani kwake Tegeta jijini Dar es Salaam wakati akijiandaa kujumuika na wanachadema kwa ajili ya maandamano.
