
Dar24 Media imetangaza kupotelewa na Mkurugenzi wake Maclean Mwaijonga ambaye mara ya mwisho kuonekana ni wakati akitoka ofisini Datavision International Ltd Mikocheni karibu na Rose Garden mnamo Oktoba 31, 2024 majira ya saa 11 jioni.
“Mkurugenzi wetu ambaye pia ni Mtendaji wa DataVision hana kawaida ya kutorudi nyumbani lakini mpaka sasa hapatikani. Wakati akitoka Ofisini alikuwa na gari aina ya Toyota Prado nyeusi yenye namba za usajili T 645 DEE.” imesema taarifa ya Dar24 Media
“Tunaomba msaada wa Vyombo vinavyohusika na Wanahabari kwa pamoja zitusaidie kupaza sauti ili kumpata Kiongozi wetu na utakapomuona yeye au gari yake tupe taarifa kwa namba hii 0713249003” — Dar24 Media