×

Somo la Mr. English lawakolea mastaa

MASTAA mbalimbali Bongo wamefunguka kuwa wanamkubali mtaalam wa Lugha ya Kingereza, Qrian James ‘Mr. English’ kwani anawapa mwanga wa kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mwigizaji Mayasa Mrisho ‘Maya’ alisema wanamkubali mtaalam huyo kwani kila anayejifunza kwake, anapata kitu kinachompa mwanga katika kazi.

“Nimepewa shuhuda mbalimbali na mastaa wenzangu, wananufaika na somo lake hata mimi nitajiunga katika darasa lake lililopo pale Sinza Lion, anatusaidia kujiweka sawa kwa ajili ya kuliteka soko la kimataifa,” alisema Maya.

Leave a Comment