×

Benki Kuu ya Uganda Yaibiwa kiasi cha shilingi bilioni 42, Maafisa Tisa Wakamatwa

POLISI nchini Uganda imethibitisha kuwashikilia maafisa tisa wa Wizara ya Fedha kwa uchunguzi wa tuhuma za kudukua mifumo ya benki kuu na kuiba kiasi cha shilingi bilioni 42 (Dola Milioni 16.87).

Haya yanajiri baada ya wizi mkubwa kutokea Novemba mwaka jana, ambapo Waziri wa Fedha, Henry Musasizi, alithibitisha kuwa akaunti za Benki ya Uganda zilidukuliwa na fedha kuhamishwa kinyume cha sheria.

Polisi imesema kuwa maafisa hao, wakiwemo kutoka idara ya hazina na ofisi ya mhasibu mkuu wa wizara, wanashikiliwa kwa ajili ya kusaidia uchunguzi wa tukio hilo.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha haikutaja majina wala idadi kamili ya maafisa waliokamatwa, lakini msemaji wa polisi, Kituuma Rusoke, amethibitisha kuwa maafisa hao wameshikiliwa na vyombo vya sheria.

Gazeti la serikali la New Vision limeripoti kuwa wadukuzi hao, waliojitambulisha kama “Taka’, walifanikiwa kudukua mifumo ya TEHAMA ya Benki ya Uganda na kuhamisha fedha hizo kwa njia haramu.

MAUAJI ya KUTISHA MWANZA: AMUUA MPENZI WAKE MWANAFUNZI wa FORM 5 NAYE AJIUA – KISA WIVU wa KIMAPENZI