
Kufuatia kuelekea uchaguzi mkuu wa Serikali unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wa 2025 katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amewasihi wanahabari kuripoti kwa weledi habari za uchaguzi, kwani sehemu nyingi wanahabari wamekuwa wakitumika kama chanzo cha uvunjivu wa amani na hivyo waendeleze ushirikiano na serikali.

Amebainisha kuwa Serikali imeendelea na jitihada za kuimarisha sekta ya elimu nchini ambapo zaidi ya madarasa 800 yamejengwa katika kipindi cha awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.