×

Mshindi wa Vazi Bora Apongeza Uzinduzi wa Heineken Silver

Mshindi wa vazi bora katika kipengele cha “Silver Futuristic” ameibuka kidedea na kitita cha shilingi milioni 2, huku akipongeza uzinduzi wa Heineken Silver – kinywaji kipya chenye ladha laini, lakini kisicho na mpinzani sokoni.

Uzinduzi huo wa kipekee ulifanyika usiku wa kuamkia Jumapili, Juni 22, 2025, katika viunga vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, na kuvutia zaidi ya wageni 400. Waliohudhuria ni pamoja na mastaa wakubwa wa Bongo, influencers wa mitandaoni, content creators wa kizazi kipya, na wapenda burudani kutoka pembe zote za jiji.

Tukio hilo lilisheheni mvuto wa kisasa, mitindo ya hali ya juu, na burudani iliyoacha gumzo, likiwakilisha mwanzo mpya kwa kinywaji cha Heineken Silver katika soko la Tanzania.