
Mama Mzazi wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli, Suzana Magufuli amefariki dunia leo Mei 25, 2026, Chato Mkoani Geita baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mtoto wa Hayati Magufuli, Jesca Magufuli amethibitisha kutokea kwa msiba huo akieleza kuwa Bibi Suzana amefariki saa 1 usiku Nyumbani kwake Chato.

“Bibi yetu (Suzana Mussa) amefariki saa moja nyumbani kwake Chato baada ya kuugua kwa muda mrefu, taratibu za msiba familia itawajulisha, Bwana ametoa na Bwana ametwaa” Jesca.