×

APR yaitumia Yanga kumpima kocha wake

YANGA (2)

Kikosi cha timu ya Yanga wakifanya mazoezi.

KATIBU Mkuu wa APR, Kalisa Adolphe amesema wanautumia mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga kupima uwezo wa kocha wao mpya, Nizar Khanfir.

Khanfir, raia wa Tunisia ana wiki moja tu APR tangu aliposaini mkataba wa miezi sita kuinoa timu hiyo na leo kwenye Uwanja wa Amahoro, Kigali ataiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza.

cecafa

Kikosi cha timu ya APR.

Adolphe aliliambia Championi Jumamosi kuwa, mchezo huo utakuwa mgumu kwa upande wao lakini watautumia kama kipimo cha Khanfir aliyewahi kuinoa timu ya taifa ya vijana ya Tunisia wenye umri chini ya miaka 23.

“Unajua tunacheza na timu kubwa Afrika Mashariki ambayo ina wachezaji wengi wenye uzoefu wa michezo ya kimataifa, lakini kwetu mchezo huu utakuwa kipimo cha kocha wetu mpya.

“Tutaangalia uwezo wake kabla ya kumuongeza mkataba mwingine hapo baadaye, nimezungumza naye mara kadhaa kuhusu Yanga, amesema hajawahi kukutana nayo lakini atajitahidi kupata ushindi,” alisema Adolphe.

Khanfir mapema wiki hii aliishuhudia APR inayomilikiwa na Jeshi la Rwanda ikiifunga AS Muhanga mabao 3-0 katika Ligi Kuu ya Rwanda kisha akaanza kuifundisha Jumanne iliyopita.

 

 

Leave a Comment