×

Video: Ajali ya Kutisha Tunduru, Lori la Mafuta Lateketea, Dereva Afariki

Dereva wa lori la mafuta, Adam Abraham (46), mkazi wa Boko-Bunju jijini Dar es Salaam, amefariki Dunia baada la gari alilokuwa akiendesha likiwa na shehena ya mafuta, kupinduka kisha kuteketea kwa moto.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, imeeleza kuwa ajali hiyo imetokea Juni 2, 2026 majira ya saa nne asubuhi katika Kijiji cha Huria, Kata ya Matemanga, Tarafa ya Matemanga, Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, kwenye barabara kuu ya Tunduru–Songea.

Ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T.833 EFY, aina ya TATA NOVUS (tanki la mafuta), mali ya Kampuni ya SOUD Industry Ltd ya Dar es Salaam lililokuwa likisafirisha mafuta ya petroli kutoka Mtwara kwenda Zambia.

Inaelezwa kuwa gari hilo liliacha njia, kupinduka na kisha kuwaka moto ambapo dereva alipoteza maisha papo hapo, kuteketea kwa gari pamoja na upotevu wa mafuta yote yaliyokuwa yanasafirishwa.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi uliomfanya dereva kushindwa kulimudu gari katika eneo lenye kona kali.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitabibu.

Leave a Comment