×

Makamu Wa Rais Nchimbi Amtembelea Rais Mstaafu Kikwete (Picha +Video)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisaliana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, katika makazi yake, Kawe Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 10 Agosti 2026.

DAR ES SALAAM: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo Agosti 10, 2026, amemtembelea na kumjulia hali Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Balozi Dkt. Nchimbi amefanya ziara hiyo katika makazi ya Dkt. Kikwete yaliyopo Kawe, jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo ni sehemu ya shughuli za Makamu wa Rais katika kuendelea kuwasiliana na viongozi wastaafu na kujua hali zao.

Leave a Comment