×

Barcelona Yaichapa Al Ahly 2-1, Yatwaa Kombe la Joan Gomper

Mabingwa wa Hispania, FC Barcelona imeifunga Al Ahly ya Misri kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Joan Gamper  uliochezwa kwenye uwanja wa Spotify Camp Nou jana Agosti 19, 2026.

Barcelona ilianza mchezo kwa kasi na kutawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza, dakika ya 29, mshambuliaji Hamza Abdelkarim aliifungia Barcelona bao la kwanza akiiweka timu yake mbele ya Al Ahly.

Barcelona iliendelea kushambulia na kupata bao la pili dakika ya 45, ambapo Raphinha alifunga kwa mkwaju wa penalti na kuifanya Barcelona kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa 2-0.

Kipindi cha pili Al Ahly ilirejea kwa nguvu na kupata bao la kufutia machozi kupitia Ahmed Sayed ‘Zizo’ dakika ya 51, goli  hilo liliifanya Al Ahly kuongeza mashambulizi ikitafuta kusawazisha lakini safu ya ulinzi ya Barcelona iliweza kuzuia mashambulizi hayo.

Barcelona pia ilipata nafasi ya kuongeza bao, lakini Anthony Gordon alikosa penalti mwishoni mwa mchezo hadi filimbi ya mwisho, Barcelona ilibaki mbele kwa 2-1 na kutwaa kombe la Joan Gamper Trophy.

Mchezo huo pia ulikuwa sehemu ya maandalizi  kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa La Liga 2026/27

Na Razaku Ramadhan.

Leave a Comment