
Kampuni ya DStv imetangaza vifurushi vipya vya huduma zake nchini Tanzania, ikiwa na maboresho yanayowawezesha wateja kupata burudani kupitia vipindi mbalimbali vya televisheni, michezo na filamu.
Kwa mujibu wa tangazo la kampuni hiyo, vifurushi hivyo vitaanza kutumika rasmi Novemba 5, 2026, vikiwa katika viwango vinne tofauti vya malipo.
Vifurushi vilivyotangazwa ni Starter kinachogharimu Shilingi 15,000, Select Shilingi 25,000, Sports Shilingi 50,000 na Ultimate kinachogharimu Shilingi 118,000.
Kupitia vifurushi hivyo, wateja watapata fursa ya kufurahia maudhui mbalimbali yakiwemo burudani za ndani na nje ya nchi, michezo pamoja na mashindano mbalimbali ya kimataifa.
DStv imetumia kaulimbiu ya “Pata zaidi na zaidi” katika kutangaza mabadiliko hayo, huku ikisisitiza upatikanaji wa burudani kupitia huduma yake ya DStv.