×

Man United Yakimbiza Kivuli cha Ferguson, Makocha 12 Ndani ya Miaka 13!

Manchester United imeendelea kukabiliwa na changamoto za kupata utulivu katika benchi la ufundi tangu kuondoka kwa kocha wake wa muda mrefu, Sir Alex Ferguson, mwaka 2013, huku mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha yakiendelea kuibua mjadala kuhusu mustakabali wa klabu hiyo.

Tangu Ferguson aondoke, klabu hiyo imekuwa chini ya makocha mbalimbali, akiwemo David Moyes (2013–2014), Ryan Giggs (2014), Louis van Gaal (2014–2016), José Mourinho (2016–2018) na Ole Gunnar Solskjær (2018–2021).

Makocha wengine walioiongoza timu hiyo ni Michael Carrick (2021), Ralf Rangnick (2021–2022), Erik ten Hag (2022–2024), Ruud van Nistelrooy (2024), Ruben Amorim (2024–2026) na Darren Fletcher (2026), kabla ya Carrick kurejea katika nafasi hiyo mwaka 2026.

Mabadiliko hayo yameifanya Manchester United kuendelea kutafuta mfumo thabiti wa uongozi wa benchi la ufundi ili kurejesha mafanikio iliyoyapata kwa muda mrefu chini ya Ferguson.

Katika hatua nyingine, klabu hiyo imetangaza kumfuta kazi kocha mkuu Michael Carrick kufuatia matokeo yasiyoridhisha katika Ligi Kuu England.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, Manchester United imekuwa na mwanzo mgumu wa msimu, ikikusanya pointi nane pekee katika michezo 10 ya ligi, ikiwa imeshinda mchezo mmoja tu na kushuka hadi nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi wenye timu 20.

Takwimu hizo zinaelezwa kuwa mwanzo mbaya zaidi wa klabu hiyo katika Ligi Kuu England tangu msimu wa 1986/87.

Kuondoka kwa Carrick kunaongeza sura nyingine katika mfululizo wa mabadiliko ya makocha ndani ya Manchester United tangu enzi ya Ferguson, huku klabu hiyo ikiendelea kutafuta namna ya kurejesha ushindani wake katika soka la England.

Leave a Comment