×

Mzamiaji harusini utamjua tu

ZAMANI ilikuwa nadra kwa mtu kuzamia kwenye harusi bila kuwa na mwaliko lakini siku hizi suala hilo limekuwa dili sana hususan harusi zile za wenye kipato cha kati. Wapo wanaozamia kwenye harusi hizo na ukitaka kumjua mzamiaji ni rahisi.

Kwanza kabla hajaenda yupo tayari kuazima suti ama sare ili aonekane ni mtu wa heshima. Muda wote akiwa ukumbini huonesha furaha hata MC akiongea kitu gani humuunga mkono kwa kupiga makofi ama kucheka, atajifanya anawajua ndugu wa bwana au bibi harusi karibu wote.

Ukifika muda wa chakula, huwa mstari wa mbele na hutumia mwanya huo kuchukua aina ya vyakula vyote vilivyoandaliwa, kila kinywaji atajaribu kukionja iwe juisi, bia, soda ama chochote na mwisho wa sherehe atafanya mbinu zote lazima atoke na kinywaji.

Leave a Comment