×

Bella azungumzia kifo cha Ndanda Kosovo ‘Kichaa’

Stori: Boniphace Ngumije
MKALI wa masauti Christian Bella ‘Obama’ amefunguka kuwa ameumizwa sana na msiba wa msanii mkongwe kwenye gemu la Muziki wa Dansi, Bongo, Ndandason Onawembo ‘Ndanda Kosovo’ kilichotokea majira ya saa mbili asubuhi, Jumamosi’ iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Bella amesema Ndanda ambaye wanategemea kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele Jumatano ya kesho jijini Dar baada ya taratibu za mazishi kukamilika, waliishi kama ndugu ambapo walisaidiana mambo mengi kimuziki na kwenye maisha.

“Jamaa alikuwa na moyo wa pekee, huwezi amini wakati mwingine alikuwa akipata shoo kutokana na ishu zake kuwa nyingi alikuwa ananiambia niende na timu yangu kukamua na wala hakutaka nimpe chochote kile, nitamkumbuka sana Ndanda, Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi,” alisema Bella.

Leave a Comment