×

Maajabu mazishi ya ndanda Kosovo

 Na Richard Bukos

MWANAMUZIKI nyota wa Muziki wa Dansi nchini, Onawembo Ngongo maarufu kama Ndanda Kosovo amezikwa katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Jumatano hii, huku maajabu ya aina yake yakijitokeza makaburini.

Wakati kwa desturi mazishi ya jamii ya Watanzania hutawaliwa na huzuni, majonzi na wakati mwingine vilio makaburini, katika tukio hilo lililojaza waombolezaji wasanii, raia wa kawaida na viongozi wa serikali, akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ndugu na wanafamilia, walikuwa wakiimba na kucheza kwa muda wote tangu walipowasili hadi mazishi yalipofanyika.

Katika mazishi hayo wanamuziki karibu wote wa bendi mbalimbali, hasa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) walikuwepo, wakiongozwa na Rais wa FM Academia, Nyoshi El- Saadat, waigizaji wa filamu, wasanii wa Bongo Fleva na wadau wengi wa Muziki wa Dansi.

Marehemu Ndanda Kosovo, aliyejipatia umaarufu mkubwa akiwa na FM Academia kabla ya kuanzisha kundi lake la Stono Musica alifariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ugonjwa unaosadikika kuwa ni vidonda vya tumbo.

Leave a Comment