×

Almasi alia na mastaa kukimbilia Sauz, Nigeria

Msanii wa Bongo Fleva anayekuja kwa kasi, Almasi Amiri ‘Almasi Masound’ amelia na mastaa wa Bongo Fleva wanao-kimbilia nchini Afrika Kusini na Nigeria kurekodi nyimbo na video kuwa kufanya hivyo kunalididimiza soko la nyumbani.

Akibonga machache na Showbiz Extra Almasi anayetikisa na Wimbo wa Baishoo ambapo kideo chake kimefanywa na Sweseka Production alisema kuwa, anaamini Bongo kuna maprodyuza na madairekta wenye uwezo wa hali ya juu kushinda huko wanakokimbilia.

“Mfano nimeshatoa nyimbo tatu hapahapa Bongo ambazo ni Nikuimbie, My, Nitunze na Baishoo, muhimu kwanza tukipende cha kwetu ili wao waje kwetu kurekodi,” alisema Almasi.

Leave a Comment