Boniphace Ngumije
ZKIWA zimepita wiki kadhaa tangu staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Moshi Katemi ‘Mo Music’ (pichani) kutemana na uongozi wake, inadaiwa kuwa meneja wake, Mack Dennis ameamua kumuangukia na kumuomba arejee kundini kama zamani.
Akinyetisha katika stori mbili-tatu na gazeti hili Mo Music alisema kuwa Mack amemuandikia barua ya kumuomba wamalize tofauti zao na kurekebisha baadhi ya vipengele kwenye mkataba lakini baada ya kumshirikisha mwanasheria wake alipinga juu ya hilo.
“Mwanasheria wangu alinishauri nisimamie maamuzi niliyoyachukua, maana kinachoonekana dhahiri huyo meneja anataka tu kunitumia na si vinginevyo, tulimjibu barua yake ambayo tulilikataa ombi hilo,” alisema Mo Music.
Hivi karibuni Mo Music alijitoa katika uongozi wake kwa madai kuwa aliishi kwa miaka mitatu bila kuona mafanikio na kwamba walikuwa wakimtumia kwa manufaa yao.
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP
*********
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz
