Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweze, Aidan Eyakuze akizungumza na wanahabari.(Hawapo pichani.)
..Eyakuze akisikiliza maswali yaliyokuwa yemeulizwa na wanahabari (hawapo pichani).
Baadhi ya wanahabri wakifutalia mkutano huo.
TAASISI ya Twaweza leo Jumanne imetoa tathimini maoni ya Watanzania Bara baada ya uchaguzi mkuu wa Visiwani Zanzibar uliofanyika Machi 20 mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari katika Ofisi za Twaweza Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Twaweza, Aidan Eyakuze amesema asilimia 53 ya wananchi wa Tanzania Bara wanasema hawafahamu kile kilichojiri Zanzibar tangu ulipofanyika uchaguzi wa Oktoba 25, 2015.
Amesema wananchi wanne kati ya 10 wanataarifa kuwa uchaguzi mpya uliofanyika Machi 20, 2016, asilimia 43 wanafahamu kuwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba yalifutwa kwa asilimia 39.
Eyakuze alisema: “Matokeo haya yametolewa na Twaweza kupitia muhtasari wa utafiti wake wenye kichwa cha habari, ‘Masuala ya Muungano: Maoni ya wananchi kuhusu kinachoendelea Zanzibar,’ muhtasari huo unatokana na takwimu zilizokusanywa na sauti za wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika kwenye uwakilishi wa kitaifa na unaotumia simu za mkononi.” Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,815 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara pasipo kuhusisha Zanzibar, kuanzia Machi 29 na Aprili 12, 2016.
Aidha, katika maoni hayo, Eyakuze alisema asilimia 42 ya Watanzania bara walitoa maoni yao kuwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein aliyechaguliwa kwenye uchaguzi wa marudio, ndiye atambulike kuwa rais halali, asilimia 20 wakisema uchaguzi huo ni hatua nzuri ya kutatua mgogoro wa Zanzibar.
Mkurugenzi huyo wa Twaweza alisema serikali ya muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zina kazi kubwa ya kurejesha umoja baina ya wapiga kura visiwani na kutia wasiwasi kubaini kwamba idadi kubwa ya Watanzania walikiri kutojua kilichotokea Zanzibar baada ya uchaguzi wa Oktoba 2015 hivyo inasababisha kuudhoofisha Muungano na kutaka wananchi kuufuatilia kwa karibu sana.
NA DENIS MTIMA/GPL