CHUCHU: GABO NI ZAIDI YA FURAHA KWANGU !

CHUCHU Hansi amefunguka kuwa, kila anapopata nafasi ya kukutana na muigizaji mwenzake Salim Ahmed ‘Gabo’ anapata amani ya moyo kwani ni mtu wanayeelewana sana.

 

Akizungumza na Amani, Chuchu anayekimbiza kunako anga la filamu Bongo, amesema Gabo anamchukulia kama kaka yake hivyo anapomuona sehemu yoyote ile lazima ajiachie na kufurahi.

 

“Mtu akitukuta na Gabo, anaweza akashangaa sana lakini ni mtuNinayeelewana naye sana hata kama nina kitu changu rohoni nakimwaga kwake,” alisema Chuchu ambaye ni mzazi mwenziye na muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’.

Stori: Imelda Mtema


Loading...

Toa comment