La Galaxy Wampa Ninja Namba 51

BEKI wa zamani wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ juzi Ijumaa alitambulishwa rasmi katika mtandao wa klabu ya La Galaxy II kama mchezaji wa timu hiyo huku akiwa amepewa jezi namba 51.

 

Ninja amejiunga na timu kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea katika timu ya MFK Vyskov ya Jamhuri ya Czech baada ya kumaliza mkataba wake wa miwili na Yanga akiwa ametokea Taifa Jang’ombe ya Zanzibar.

 

Ninja alitambulishwa katika mtandao rasmi wa timu hiyo ambao unahusika kutoa taarifa za timu hiyo anayocheza mshambuliaji wa zamani wa Barcelona na Manchester United, Zlatan Ibrahimović.

Akizungumza na mtandao huo, meneja mkuu wa timu hiyo, Dennis te Kloese alisema kuwa wamesaini beki huyo kutoka Tanzania kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu akitokea katika klabu ya MFK Vyskov huku akiwa tayari ameshapa kibali chake cha uhamisho wa kimataifa ITC na kibali cha kufanyia kazi nchini maarufu kama P1 Visa.

 

“Tumemsajili Abdalla (Ninja) katika orodha ya wachezaji wetu kwa ajili msimu ujao wa ligi, Abdallah ni
bado ni beki kijana mdogo mwenye uwezo mkubwa hapo baadaye, tunamuangalia kwa ajili ya kuendelea na timu yetu,”alisema Beki huyo jana Jumamosi alitarajia kuwa sehemu mechi ya kirafiki kati dhidi ya New Mexico United uliopangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Isotopes Park, Albuquerque.


Loading...

Toa comment