The House of Favourite Newspapers

NAY Afunguka Mazito Baada ya Kuitwa BASATA – Video

RAPA marufu nchini Emmanuel Elibariki ‘Nay wa mitego’ jana Oktoba 23, 2018 alifika katika ofisi za Baraza la Sanaa la Tanzania ‘Basata’ kwa ajili ya kuitikia wito ikiwa ni siku chache baada ya kuachia wimbo wake mpya unaoitwa Alisema.

 

Nay ambaye amekua akiachia nyimbo mbalimbali zenye maudhui ya kuikosoa na kuikumbusha Serikali kutekeleza baadhi ya majukumu yake kwa wananchi wake, amesema aliitwa kwa ajili kujadiliana na kupewa elimu mbalimbali juu ya utungaji wa mashairi yake.

 

Hii ni zaidi ya mara tatu au nne Nay amekuwa akiitwa BASATA kuonywa na wakati mwingine anaamriwa kubadili baadhi ya mashairi katika nyimbo zake mfano wimbo wa WAPO ambao aliamriwa na Waziri wa Sanaa, Dkt. Harrison Mwakyembe kubadili mashairi kwa agizo la Rais John Magufuli ili uendelee kupigwa redioni.

 

Baada ya kuitwa jana, msanii huyo amesema wimbo wa ALISEMA haujafungiwa bali ulikuwa ni mjadala ambao Basata ama TUMA (Shirikisho la Wasanii) watalitolea ufafanuzi kwani yeye siyo mzungumzaji.

MSIKIE NAY AKIFUNGUKA – VIDEO

Comments are closed.