MOSHI: Mchekeshaji mahiri, Katarina wa Karatu, amefungukia kifo cha mzee Ndesamburo, akieleza kwamba ameguswa sanana msiba huo kutokana na jinsi alivyokuwa akiishi na watu na kufunguka kwamba yeye ndiye aliyemshawishi kuingia kwenye siasa.
Katarina anasema katika maisha yake, amewahi kukutana na ndesamburo mara moja na kamwe hawezi kusahau moyo wa upendo aliokuwa nao katika kusaidia watu.
Amesema kwamba baada ya kuingia kwenye siasa, alijiunga na Chadema ambayo Ndesamburo pia alikuwa mwanachama wake mkongwe na kueleza kwamba yeye na wachekeshaji wenzake wanafikiria kuandaa siku maalum kwa ajili ya kumuenzi.