×

Bayo Na Imbori -30

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Akiwa kwenye chumba katika uangalizi maalumu Hospitali, Imbori anachomwa sindano yenye madini ya chumvi-sumu yaitwayo Acetate ukiwa ni mchongo alioupanga Josephine kwa lengo la kummaliza msichana huyo baada ya kuponea chupuchupu alipopigwa risasi.Tambaa nayo…

MADINI ya chumvi-sumu aliyochomwa Imbori yanasambaa kwenye mwili wake, kwa kasi ya ajabu anapoteza kiwango kikubwa cha maji kiasi kwamba hata Dk. Donard Mand alipokwenda kumjulia hali alishangazwa na upungufu huo.

Aliwauliza manesi nini kilitokea hadi mgonjwa huyo akawa katika hali hiyo lakini hakuna aliyekuwa na jibu. Jambo hilo lilimfanya ahisi kuwepo na kitu ambacho hakikuwa sawa miongoni mwa wasaidizi wake.

Kutokana na uzoefu wa kazi aliokuwa nao, kwa kumtazama Imbori aligundua msichana huyo alikuwa na tatizo la kuishiwa maji kwa kiasi kikubwa jambo ambalo alifahamu halikuwa likiwezekana kutokea kwa kasi kama ilivyokuwa. Dk. Mand akaamua kuwa mpole ili kwanza ayaokoe maisha ya mgonjwa kisha baadaye alishughulikie hilo.

Alichokifanya haraka ni kumfanyia vipimo vya mwili mzima Imbori ambapo majibu yalionesha kuwepo na sumu hatari ya Acetic Acid kwenye mzunguko wa damu yake. Bila kupoteza muda, akamfanyia huduma ya kitaalamu inayoitwa Dialysis yaani njia mbadala ya kuondoa uchafu uliozidi mwilini (Excess Waste Products), baada ya huduma hiyo aligundulika pia figo moja ya Imbori ilikuwa imeharibika vibaya.

“We have to remove her kidney immediately,” (Tunatakiwa kuiondoa figo yake mara moja) Dk. Mand alimwambia Dickson baada ya kumpa majibu ya vipimo.
“Is there no any other alternative we can use instead?” (Hakuna njia nyingine yoyote mbadala tunayoweza kutumia?)

“No; acetic acid is very hazardous it destroys the kidney faster. However, she can live by undergoing periodical dialysis if you can’t afford to provide her with another kidney.” (Hapana, Acetic acid inaharibu figo haraka, lakini anaweza kuishi kwa kusafishwa damu ikiwa huwezi kumudu gharama za kupata figo nyingine.)

“How does it cost?” (Inagharimu vipi?)
“It’s too expensive.” (Ni ghali mno)
Dk. Mand na Dickson waliendelea kujadiliana juu ya hilo, mwisho walikubaliana kumbadilisha Imbori figo maana pesa kwa Dickson halikuwa tatizo na alichokuwa anahitaji ni kumuona mpenzi wake anapona tu.

Ili kufanikisha hilo waliweka matangazo kwenye mtandao wa wachangia figo maarufu duniani uitwao www. Kidneydoner.uk.com, lakini watu takriban mia moja waliojitokeza hawakuwa na sifa ya kumbadilishia figo Imbori.

Jambo hilo lilimsikitisha sana Dickson, pesa haikuonekana kuwa msaada kwa msichana aliyempenda kutoka kwenye mateso makali yaliyokuwa yanamkabili, hali yake ilizidi kubadilika kila sekunde jambo lililoashiria angekufa ndani ya siku chache zilizofuata.

“I wanna donate my kidney,” (Ninahitaji kumchangia figo yangu) Dickson alimwambia Dk. Mand baada ya kuona hali ya Imbori inazidi kuwa mbaya.
“Sure?” (Kweli?)

“Exactly, I love her so much.” (Hakika, nampenda sana.)
Dk. Mand hakuwa na neno lolote la kuongeza, alichomwambia Dickson ni kumsihi kufikiria mara mbili juu ya uamuzi wake maana kutenda jambo hilo kulimaanisha kuyahatarisha maisha yake. Hata hivyo, Dickson hakujali juu ya hilo, alichohitaji kuona wakati huo ilikuwa ni Imbori kupona na kurudia hali yake.

Vipimo kwa Dickson juu ya afya yake vilifuata kabla ya kusaini karatasi za kukubali kufanya upasuaji wa figo, kwa bahati mbaya hakuonekana kuwa na sifa za kumchangia figo Imbori, jambo lililozidisha maumivu kwa kijana huyo. Imbori kukosa figo kulimaanisha kifo, kila siku walikuwa wanamchuja damu lakini hakuonesha kupata unafuu wowote ule.

Bila kukata tamaa Dickson aliongeza dau kutoka lile alilokuwa amelitangaza mara ya kwanza la dola milioni 200 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi bilioni 400 za Kitanzania, zikafikia bilioni 500 pia mbali na www.

kidneydoner.co.com, tangazo hilo walilipeleka kwenye Mtandao wa Gossip Cop, uliokuwa unasomwa na watu wengi zaidi duniani, baada ya siku mbili akapatikana kijana aliyejitambulisha kwa jina la Bayo kutoka nchini Tanzania.Je, nini kitaendelea?  Usikose wiki ijayo.

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO, BOFYA HAPA ===>https://www.facebook.com/shigongotz/

Leave a Comment