KAMA kawa, kama dawa. Mpenzi msomaji tunaendelea kuwatembelea mastaa mbalimbali nyumbani na kuona namna ambavyo wanaishi na shughuli wanazozifanya.
Leo tumemtembelea Miss Ruvuma 2006, Isabela Mpanda ‘Bella’. Anaishi na msichana wa kazi nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar. Ana watoto wawili lakini wote wanasoma ‘boarding’.
Baada ya kumpiga picha kadhaa, mwanahabari wetu alianza kumuuliza maswali mawili matatu;
Mpaka Home: Ratiba yako ikoje asubuhi? Unaamka saa ngapi?
Isabela: Naamka saa 2 nakunywa kikombe kimoja cha maji ya moto yenye ndimu halafu nakwenda kuwapa kuku chakula. Baada ya hapo nakwenda kwenye shuguli zangu za muziki.
Mpaka Home: Una kuku wangapi? Nani anawahudumia?
Isabela: Kuna mkaka anawahudumia ila hata mimi mwenyewe na msichana wangu wa kazi huwa tunawahudumia. Kuku wapo 19. Ni wa kienyeji.
Mpaka Home: Kwa nini unaweka ndimu kwenye maji ya moto au mambo yetu (bia)?
Isabela: Hahahaha! Si hayo tu bali si unajua mimi sitaki unene, nakunywa ndimu sababu ya kukata unene.
Mpaka Home: Mbona simuoni mpenzi wako Luten Kalama hapa nyumbani?
Isabela: Yule tumeshindwana muda mrefu, kwa sasa nipo mimi na msichana wangu tu wa kazi.
Mpaka Home: Inamaana kwa sasa hakuna mpenzi anayekupa kampani uwapo nyumbani?
Isabela: Siishi na mpenzi ila nitatoa tamko ‘soon’ kwani nina mipango ya kurudiana na baba mtoto wangu kama atanikubalia. Ila msijali tamko linakuja soon!
Mpaka Home: Vipi kuhusu nguo za ndani, anakufulia dada au unafua mwenyewe?
Isabela: Nafua mwenyewe ila kila baada ya mwezi ndiyo nafua. Yaani nikioga natupa kwenye kapu ikifika mwisho wa mwezi ndiyo nafua.
Mpaka Home: Biblia huwa unasoma muda gani wakati najua muda mwingi unakuwa viwanja?
Isabela: Nasoma kabla na baada ya kulala. Nimetulia sana siku hizi sitoki ‘out’ mara kwa mara kama zamani. Biblia nimeanza kusoma tangu nikiwa darasa la tatu kipindi napokea Komunio ya Kwanza.