Stori: Mayasa Mariwata
Ilikuwa juzikati ndani ya Ukumbi wa Club Bilcanas ambapo mwanadada mwenye figa f’lani bomba, Gigy Money juzikati alipanda jukwaani na kuimba sambamba na msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Abdu Kiba.
Kilichowavutia wengi waliokuwa ukumbini hapo ni staili yao ya uchezaji kwani Gigy alikuwa akimkatia Kiba mauno huku kukumbatiana ikiwa sehemu ya shoo hiyo.
Awali alipanda Ali Kiba kumpa mdogo wake kampani, aliposhuka Gigy naye akapanda na kukamata mic ambapo licha ya kuonesha umahiri wa kuimba, burudani kubwa ilikuwa yale malovee waliyokuwa wakiyaonesha walipokuwa wakipafomu.