×

Mama Diamond Amtoa Chozi Esma Mahakamani

Na MWANDISHI WETU| GAZETI LA IJUMAASTAR MIX

MAMA wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’ hivi karibuni alimtoa chozi mwanaye Esma Abdulkadiri walipokuwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar walipoenda kufuatilia kesi za watu wao wa karibu, Ahmed Hashim ‘Petit Man’ na Romeo Bangura ‘Rommy Jons’ waliokuwa wakikabiliwa na msala wa madawa ya kulevya.

Wakiwa mahakamani hapo, mama Diamond alionekana kumnong’oneza kitu Esma, ghafl a hali ikabadilika ambapo Esma ambaye ni mke wa Petit alianza kulia huku wakati mwingine akitumia mtandio wake kujifuta machozi.

Bila kujulikana aliambiwa nini kilichompa machungu, mama Diamond alianza kumbembeleza na baada ya muda akatulia na kuendelea kufuatilia kesi mahakamani hapo. Hakuna aliyeweza kupatikana mara moja kuzungumzia hali hiyo. Mama Diamond alifi ka mahakamani hapo kufuatilia kesi ya mkwewe (Petit) na mwanaye Rommy huku Esma akienda kwa ajili ya mumewe (Petit) na kaka yake (Rommy).  MAMA

Save