MTOTO wa mchezaji soka wa zamani wa Brazil, Edson Cholbi do Nascimento, amesema baba yake, Edson Arantes do Nascimento ‘Pele’, mwenye umri wa miaka 79 ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo la nyonga kwa muda mrefu sasa ana hofu ya kutoka nje ya nyumba kwani anaona aibu kutokana na hali yake ya afya kuwa mbaya.
Pele ambaye ana rekodi ya kipekee duniani katika tasnia ya soka, alifanyiwa upasuaji wa nyonga lakini hakupata muda wa kupona vizuri, hali iliyomsababishia tatizo la kushindwa kutembea bila usaidizi na kumshinikiza kiakili.
