RAIS John Magufuli amemfukuza kazi kijana aliyechana kitabu kitakatifu cha Quran mkoani Morogoro, Daniel Maleki, na amemuagiza Waziri was Tamisemi, Suleimani Jafo kumuandikia barua ya kumfukuza kazi.
Magufuli amefanya uamuzi huo leo Jumanne, Februari 11, 2020, eneo la Gezaulole, Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam wakati akihutubia baada ya kuzindua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni na jengo la Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni.
“Juzi nilikuwa namsikia Mheshimiwa Jafo, mtu mmoja kule Kilosa nafikiri alichana kitabu kitakatifu, nashukuru umechukua hatua ya kumsimamisha kazi. Lakini mimi namfukuza moja kwa moja, mwandikieni barua ya kuondoka moja kwa moja.
“Ashinde kesi, asishinde huyo siyo mfanyakazi wa serikali. Hatuwezi tukakaa na wafanyakazi wapumbavu katika serikali hii. Umechukua jukumu la kumsimamisha kazi lakini mimi namfukuza,” amesema.
