Ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali katika kujikinga na maambukizi dhidi ya virusi vya Corona, Serikali Mkoani Kilimanjaro imepanga kufanya zoezi la upuliziaji dawa kwenye maeneo mbalimbali Mkoani humo ikiwa ni mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.
Akiongea wakati wa makabidhiano ya vifaa vya usafi kutoka kwa taasisi ya Vijana Kwanza vyenye thamani ya shilingi milioni tano, Mkuu wa Wilaya ya KIlimanjaro Kippi Warioba ameishukuru taasisi hiyo na kutoa wito kwa jamii kuunga mkono mapambano dhidi ya virusi vya Corona huku Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Michael Mwandezi akielezea utekelezaji wa zoezi la kunyunyiza dawa kwenye vyomba vya usafiri.