
HAJI Manara amesema amemueleza wazi Jerry Muro ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kuwa akiendelea kumfuatafuata atavunja ndoa yake. Manara ambaye ni msemaji maarufu zaidi wa klabu za soka nchini akitokea Simba, amesema alimueleza Muro waziwazi kuwa ana siri zake nyingi ambazo akizitoa ni hatari kwa nchi na zitavunja ndoa yake.
Katika mahojiano maalum na Spoti Xtra, Manara amesema: “Sijawahi kuwa na urafi ki na Jerry Muro, ni mdogo sana kwangu. Nilikaa kimya tu kwa kuwa mamlaka iliyomteua kwa maana ya Mheshimiwa Rais, ninamheshimu sana. “Nakumbuka nikiwa Ulaya nikaona anaendelea kuzungumza mambo mengi.
Saa tuna kundi letu la kamati ya timu ya taifa, akaandika ujinga wake. Waulizeni walio kwenye kamati hiyo watawaambia. “Nilimjibu mule, nikamjibu na kumueleza hiyo ni kidogo, najua nilichomueleza. Nikampigia yeye na kumuambia aseme tena aone, nitasema kila kitu hadharani, akifyatua nafyatua kudadadeki.
“Akaniambia ataenda TCRA, nikamuambia atangulie na mimi ntafuatia kwa kuwa nina ushahidi wa yeye alivyonisema mambo yake ya hovyo.
“Nasema hivi akisema tu nafyatua, nina siri kubwa ya Muro. Akisema tu nafyatua na ninakuambia leo, kesho Rais anamtengua tu.
Sina kawaida ya kuheshimu hawa watu na vyeo vyao, ila mimi ninamheshimu Mheshimiwa Rais. “Jerry anawezaje kuwa kiboko yangu, mtu asiyejua mpira hata kidogo, hajui chochote.
Kaniita msukule, ndio tusi. Natukanwa kila siku, kama uandishi nimeanza kabla yake. “Ila nasisitiza akisema nitatoa siri zake zote za ndani, nitamfyatua na ndoa yake nitavunja.”