×

Corona: Wagonjwa 6 Waongezeka Zanzibar, Mmoja Afariki

WIZARA  ya Afya Zanzibar imetangaza wagonjwa wapya sita wa virusi vya Corona na kufikisha idadi ya wagonjwa 18 kutoka 12 walioripotiwa awali Aprili 13, 2020, Visiwani humo.

 

Miongoni mwao, wagonjwa watano ni wanaume na mmoja ni mwanamke na hawana historia ya kusafiri nje ya siku za hivi karibuni. Pia yumo raia mmoja wa Misri hivyo kufanya jumla ya watu walioambukizwa corona kwa nchi nzima (Tanzania Bara na Zanzibar) kufikia watu 59.

 

Taarifa iliyotolewa leo na Wizara hiyo inasema kuwa, mmoja wao alifariki Aprili 11, 2020.

Leave a Comment